Habib Haji ameibuka mchezaji bora wa wiki baada ya kiwango bora wikendi iliyopita - Goal.com

Goal.com

HomeScores

Habib Haji ameibuka mchezaji bora wa wiki baada ya kiwango bora wikendi iliyopita

Jan 1, 2018 12:41:49Main
Mshambuliaji wa Mbao Habib Haji amefanikiwa kuwa mchezaji bora wa wiki baada ya kuwa kwenye kiwango bora dhidi ya mabingwa watetezi klabu ya Yanga

Habib Haji ametimiza magoli 7 kwa msimu huu mpaka sasa huku akiwa nyuma kwa goli moja dhidi ya kinara wa magoli, Emmanuel Okwi mwenye magoli 8 hadi sasa

Habib Haji amefanikiwa kuibuka nyota wa wiki kufuatia kiwango bora alichoonesha dhidi ya Yanga, straika huyo ndiye aliyepeleka msiba kwa Wana jangwani baada ya kuwatungua magoli mawili na kuiwezesha klabu yake ya Mbao Fc kuibuka na ushindi wa goli 2 kwa 0 dhidi ya mabingwa hao watetezi

Haji alifunga magoli hayo kwa ustadi mkubwa sana hasa goli la kwanza alilofungwa kwa umbali wa mita 25 baada ya kuwaramba chenga mabeki wa Yanga kisha kuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Yanga, Youthe Rostand 

Habib Haji amefanikiwa kushinda tuzo hiyo baada ya kuwazidi nyota wengine waliokuwa na kiwango bora wikendi iliyopita kama John Bocc, Jonas Mkude, Salmin Hoza, Salum Kimenya na wengineyo 

Baada ya mechi za wikendi iliyoisha Ligi Kuu inatarajiwa kusimama kidogo kupisha michuano ya Mapinduzi inayofanyika visiwani Zanzabar


Next Article

Sterling receives Integrity and Impact Award for stance against racismSterling receives Integrity and Impact Award for stance against racism
4/26/19


Related

Sterling receives Integrity and Impact Award for stance against racismSterling receives Integrity and Impact Award for stance against racism
Gerrard's cousin Duncan on target as Liverpool beat Man City to win FA Youth CupGerrard's cousin Duncan on target as Liverpool beat Man City to win FA Youth Cup
Getafe 0 Real Madrid 0: Zidane's men held by Champions League chasersGetafe 0 Real Madrid 0: Zidane's men held by Champions League chasers
HomeScores